Maana kama Vile mbegu hupandwa na kutoa mmea ndivyo ambavyo Kila Neno lililopandwa kwa Ufunuo ndani ya Moyo wa mwanadamu huzaa Utukufu katika Mwili Wa ufufuo.

Mungu katika Roho Matakatifu Husafishwa mwili wa Mauti ili Katika muda wa ufufuo wa wafu Uzima Upatikane katika Uhalisia Mpya utakaofunuliwa

Kutokana na Kwamba Msingi wa Kuishi katika mwili umekuwa na makosa katika kufundishwa kwake basi Msingi wa maisha Nje ya Mwili huu vivyo hivyo umekosa Fasili.

Lakini ni muhimu kanisa kunia sana kuijua Mauti kama ambavyo linatazamia Uzima, maana Uharibifu huanza kwanza na baadaye Kutokuharibika, Uzima kwa Kujua Kwanini Mungu alimpa nafasi mwanadamu ya Kuishi katika Mwili, na Mauti kwa Kutimiliza Kusudi la Kusihi katika mwili.

Mambo haya mawili hubakia kama kioo kwa wale waliokubali Kuzaliwa kwa Neno la Mungu ili Ushirika wao na Mungu uthibitishwe katika haki na Kweli.

Mwanadamu , Furaha yako Iwe Katika Kumjua Mungu na Tathimini ya maisha yako isiwe katika yale uliyoyafanya Bali Mungu aliyefanyika ndani Yako, Kaa katika Toba ili Nuru ithibitishwe katika Uzao wa Mungu ndani ya Kristo Yesu.

Mungu Akubariki.

Recent Posts

Leave a Comment

Contact Us

We're not around right now. But you can send us an email and we'll get back to you, asap.

Not readable? Change text. captcha txt