Kumfundisha mwanamke kujua nafasi yake katika Jamii, mwanamke kujua ya kuwa yeye sio dhaifu anaweza akafanya mambo makubwa, wanawake na sisi tunaweza, Mwanamke anaweza akafanya kazi za mwanaume na kuwa katika nafasi mbalimbali ambazo wanaume wamekuwa wakisimama siku zote..

Hizi ni kelele kutoka katika kila kona ya Dunia, wanawake wakiwa katika Moto wa kupokea uwezo ambao ndo wanafahamu kuwa wanao duniani kote, katika Nyanja za Dini na Katika Nyanja za Kijamii na katika Nyanja za Kiroho.

Mungu anasemaje Kuhusiana na Hili?

Sasa hapa nitaongea na kanisa, Mungu ni wa wote lakini Njia ya ufunuo Kumfikia Yeye katika usafi wote na imani hupatikana kwa kanisa, Ndio maana nitasema na waamini , lakini Pia nasema na waamini kwa sababu ya Unabii ambao Mungu kupitia Roho Mtakatifu anauthibitisha hata sasa.

Mwanzo 3:

Akamwambia Mwanamke Hakika Nitakuzidishia Uchungu wako na kuzaa kwako, kwa utungu utazaa watoto na tamaa yako itakuwa juu ya mume wako naye Atakutawala.

Kuna mambo kadhaa natamani Kuyaaijisha hapa kwa ajili ya kutusaidia…

1. Kutawaliwa kwa Mwanamke ni Amri iliyokuja kama Laana Kutoka kwa Mungu.

2. Laana Imekuja baada ya mwanamke kukosa Kutii Nafasi yake ya Kimamlaka

3. Mwanaume Hajataka Kumtawala mwanamke bali Mungu ameamuru iwe hivyo.

Mambo hayo Matatu juu ni ya Msingi sana Kuyafahamu ili kuhakikisha kuwa katika Nyakati hizi mwanamke anapodai kutoka katika Utawala wa Mwanaume au anapodai kuwa huru anatakiwa Ayafahamu ili Kanisa lisipotee katika Upuuzi wa Kimapokeo ya Kijamii na kuiacha Njia ya Kweli ya Kiroho.

Mifumo Roho inayoratibu Hali ya Mitazamo katika mwili imekaa kwa namna Hii..

1. Adam wa kwanza
2. Adam wa pili

1. Adam kwa kwanza.

Kupitia Adam kwanza na mfumo wake w umiliki katika Ulimwengu Ndipo mwanamke anawekwa chini ya Utawala wa Mwanamume, Lakini amri hii haikuwa kwa wale walio wa jamii ya Adamu tuu lakini katika Mfumo mzima wa Ulimwengu ukaakisiwa na Amri hii, hii ni kwa sababuvya nafasi ua Kiumiliki ya Adamu katika Ulimwengu.

Ndio maana Biblia inaandika ya kwamba viumbe vyote Vinaugua vikitazamia kufunuliwa kwa wana wa Mungu, Ikia inalenga kuonesha mfumo wa Ulimwengu ulivyoharibiwa

2. Adamu wa Pili.

Kupitia Adamu wa Pili Mifumo inarejeshwa katika Hali yake ya kwanza na maana yake pia katika Mwanamke kuna jambo linatengenezwa. Na kwa sababu Ninaongelea suala la Mwanamke kuwezeshwa Nitajikita Hapa katika Kudadavua.

Mfumo wa Mwanamke unatengenezwa katika mambo Yafuatayo

1. Uchungu wa Mwanamke Kuongezeka katika Kuzaa watoto

2. Tamaa ya Mwanamke kuwa kwa Mwanaume

3. Mwanamke kutawaliwa na Mume wake.

Mambo haya matatu yalikuwa ni Laana kwa sababu ya kosa, Hivo Adamu wa Pili anapofunuliwa Huyabadilisha haya kwenye mfumo wake katika ulimwengu wote.

Lakini kwa Wewe Mkristo ambaye ni Kuhani wa Mungu ni lazima ufahamu ya kwamba hakuna Laana ambayo inakuja katika maisha ya mwanadamu Bila kanuni lakini zaidi Hakuna laana ambayo inaondolewa bila kanuni.

Lakini pia Jambo kubwa la kujiuliza ni kwanini Mungu anatoa Amri ya namna hiii kwa mwanamke, na Kwa kufahamu hivo itakuwa ni rahisi sana kwetu kuelewa namna ya kutoka hapo katika zama hizi za Adamu wa pili. Hivo Tunapoona Kuwezeshwa kwa mwanamke kunakopiga kelele sio suala la utandawazi lakini ni suala Kinabii lililotokana na Mungu halitakiwi kuchukuliwa kisiasa au Kikawaida bali Kiroho na kwa umakini maana humtoa Mwanamke kwenye laana itokanayo na Mungu

MUNGU ATUPE KUJUA NA KUONA

Sehemu ya 02

Sehemu iliyopita nilijitahidi kuonesha mambo kadhaa ambayo kanisa linatakiwa kuyatazama linapokuwa katika Mfumo wa Uwezeshwaji wa mwanamke kama ambavyo leo unaitwa.

Kumbuka Nilianisha mambo ambayo Yalitamkwa kama Laana na Mungu mwenyewe juu ya mwanamke, Nikasema
1. Uchungu Kuongezeka wakati wa uzao
2. Tamaa ya mwanamke kuwa kwa mwanaume
3. Na mwakamke Kutawaliwa na Mwanamume.

Haya yote katika Mfumo mpya wa Kristo Yesu yanatakiwa Yasiwepo kwa Mfumo huu

1. Uchungu wa kuzaa Upunguzwe na urejee Katika Hali ya Awali 
2. Tamaa ya Mwanamke isiwe kwa Mume wake
3. Na mwanamke Asitawaliwe na Mume wake.

Leo Nitaelezea kwa uchache mambo ya kuzingatia wakati mwanamke anawezeshwa au anakombolewa kikanuni kutoka katika mambo hayo Husika.

1. Jambo la kwanza la Kujua ni Kuwa Mwanamke anapojikwamua katika Haya , Hajikwamui Kutoka kwa Mwanaume bali Mungu.

Kama kanisa ni lazima tufahamu kanuni za Kufunguliwa Kutoka kwenye Laana ambayo ilitolewa na Kinywa cha Mungu.

Kanuni la Ukombozi ndiyo iliyomfanya Kristo Yesu yaani Mungu ajifunue katika mwili na Kuupatanisha Ulimwengu kwa Nafsi yake, Je unafikiri Ni kwanini Muumba ambaye ni Mtawala wa Kila kitu ajinyenyekeze katika yale aliyoyaumba ili ayaletee amani? Kanuni ndizo ambazo zikisababisha haya.

Hivo mwanadamu ni lazina afahamu Jinsi kanuni zinatebda kazi ili aweze Kufahamu njia sahihi ya Kuyapokea yaliyo kamili kutoka kwa Mungu.

Hivo Mwanamke ni Lazima afahamu ya kuwa Kama anataka Kuwa na Nguvu na uwezo katika jamii ni lazima Arudi kwenye Mfumo wa Kudhoofishwa kwake, na chimbuko la mfumo huu ni Laana kutoka kwa Mungu.

Kwa maana hiyi napenda kusema kuwa katika Tendo au movement ya Kuwezeshwa mwanamke Adui sio Mwanaume bali Mungu, Mwanaume hakutaka kumtawala mwanamke bali Mungu alimtawalisha mwanamke chini ya mwanaume tamko la laana.

Jamii inatufundisha kuona Uadui wa kudhoofishwa kwa mwanamke kana kwamba ni Tendo la Mwanaume ,.lakini Biblia inatuonyesha ya kuwa jambo hili ni Njia ya Mungu kwa kosa la Kutokutii.

Mwanamke na ajifunze kushindana na Mungu katika hili na si kushindana na mwanaume. Ni Kosa la kikanuni na lina madhara makubwa Kiroho na katika uhalisia uabudu katika mwili wa Kristo.

Baadaye kidogo nitaonyesha Jinsi kosa hili la Kikanuni linaruhusu Kurudiwa kwa Kosa ambalo Hawa alifanya , Yaani mwanamke sasa akikosea kanuni hii basi hata katika zama hizi za Ufunuo wa Mwana wa Mungu anarudia kosa lile lile kwa Kuufanya Uzao Ulionunuliwa Kwa damu ya Yesu kuzaliwa tena katika Mfumo wa Giza na Mauti.

Hivo kanisa kama watu ambao tumetengwa, ufahamu wetu lazima uwe safi ili kuhakiki uweza wa Mungu na Mbegu safi katika Kusudio la Mungu na uzima wa Milele.

Katika sehemu inayofuata nitaeleza Jambo la pili ambalo ni Muhimu pia kuangaliwa ili Kufikia siri ya usafi wa Ukombozi kutoka katika Jambo hili.

Mungu Akubariki.

Recent Posts

Leave a Comment

Contact Us

We're not around right now. But you can send us an email and we'll get back to you, asap.

Not readable? Change text. captcha txt