Mfumo wa Kusudi la Kuishi linapatikana ndani ya Mtu mmoja Adam wa kwanza.

Tukitaka kufahamu Maana ya maisha ambayo tunaishi au kwanini tunasema sisi sio wa Ulimwengu huu basi ni lazima tufahamu namna ya kuuendea uhalisia huu ambao Mungu ameuficha ili Watakaoitambua siri hii waitwe Wafalme.

Nimesema Kusudi la maisha linapatikana kwa Mtu mmoja Adamu wa kwanza, maana katika huyu Mausia ya kuuvaa mwili na kuwapo katika Ulimwengu huu yaliachiliwa.

Adamu wa Pili yaani Yesu Kristo anapokuja yeye anakuja kurudisha kile kilichopotea kwa maana ya kwamba anarudisha msingi uliowekwa na Mungu aliye hai katika Adam wa kwanza.

Tusichanganye Mfumo wa Ukuaji na Mausia ya Kukua. Kristo Yesu ni Mfumo ukuaji kumfikia Mungu, Ni njia Pekee kuufikia Ukamilifu wa Mungu asiyeonekana lakini Adamu wa Kwanza ni Malimbuko ya Kuingia katika Mfumo ambayo ni Yesu Kristo.

Ndio maana hata yeye Mwenyewe Bwana Yesu anapofunuliwa duniani anakuja Kurudisha Kile ambacho kilipotea kwa Adamu wa Kwanza.

Tukitaka kufahamu Kusudi la Uhai Hatujifunzi kutoka kwa Yeyote bali Adamu wa Kwanza ili Kuyafikia Mausia ya Kumpokea Adamu wa pili Yesu Kristo katika Kukamilisha Maana ya Kukaa katika Nyumba hii ya mwili. Kila kitu ambacho Mungu amekifanya , kimewekwa katika mfumo sahihi ili kumfanya mwanadamu atembee katika mapenzi makamilifu ya Mungu.

Jikite katika Kuyatafakarii Haya.

Recent Posts

Leave a Comment

Contact Us

We're not around right now. But you can send us an email and we'll get back to you, asap.

Not readable? Change text. captcha txt