Katika Nafsi ya mwanadamu, Mungu ameweka nguvu ya kufikiri (Imagination). Jambo hili humfanya mwanadamu awe na uwezo wa kuumba yale mambo ambayo hayapo katika ulimwengu wake. Lakini pia humfanya mwanadamu awe na uwezo wa kuyaona yale yasioonekana na kuyaleta kuwa matendo katika Ulimwengu huu wa mwili.

Kama Unaweza Ukafikiri Matatizo Yako Mpaka Ukaugua Vidonda Vya tumbo au Ukapata Blood Pressure au Ukaumwa na Msongo wa mawazo au Ukachanganyikiwa Kabisa na Mfumo wako wa maisha Ukaharibika.. Magonjwa haya yote huwa yanatengenezwa na nguvu kubwa ya Tafakari ambapo mwisho wake hutengeneza kitu halisi kama vidonda vya tumbo. Lakini ili tafakari ilete kitu halisi namna hii ni lazima iwe ni tafakari inayofanyika kwa Mfululizo (consecutive)

Kwahiyo kama unaweza kutafakari mpaka ukatengeneza magonjwa ndani yako Basi unaweza Kwa namna hiyohiyo ukalitafari Neno la Mungu Ukatengeneza uponyaji ulio halisi, Ukaisikia sauti ya Mungu kwa Usahihi, Ukawahudumia watu wengine kwa kutangaza Uponyaji Juu ya maisha ya wengi, ukaiponya nchi kwa sababu ya kufikiri Huko, Aisee ukamruhusu Mungu kuishi katika mwili kupitia Kulitafakari Neno lake la Milele…

Natamani tujifunze kulitafakari Neno la Mungu, Zaidi ya tunavyotafakari Jambo lingine lolote..

Kutafakari kunaweza kukazalisha jambo ambalo ni halisi kwa namna ya mwili likewise Uwepo wa Roho Mtakatifu ni Zao la kutafakari …

Jikite kwenye Tafakari. Barikiwa sana.

Recent Posts

Leave a Comment

Contact Us

We're not around right now. But you can send us an email and we'll get back to you, asap.

Not readable? Change text. captcha txt