Fundisho la siku za Mwisho 1

Kanisa la Mungu katika Yesu Kristo katika mwanzo wake yaani katika kipindi cha mitume lilijikita katika kupambanua maono ya Injili yaani kumpevusha mwanadamu katika Ufahamu wa mwana wa Mungu ili basi Mwanadamu katika Yesu kristo apate kupita kutoka katika nguvu za mauti na utawala wake katika namna zote.

Maana yake ni lazima atakaswe kwa neno ili asije akapotoshwa na uharibifu ambao umepatikana katika dunia. Na hapa ndipo fundisho la siku ya mwisho linatakiwa litambulikane kwa Kiwango cha juu sana katika kanisa.

Majira ya nyakati hubakia duniani na watu tofauti tofauti huishi katika hayo, hivo kama katika nyakati mojawapo jambo lolote likibadilishwa na kukosewa basi katika vizazi vijavyo litakuwa ndio sheria.

Kanisa letu katika kipindi hiki limejikita katika ufafanuzi wa jinsi uweza wa Mungu umejikita katika maisha ya mwanadamu , kwa kuzingatia maono na mfumo mzima wa jinsi Mungu anaweza akajidhihirisha kwa ukuu wake kwa wale wanaomwamini, lakini Fundisho la kuyatambua majira na nyakati halijawa na nguvu nadhani ni kwa sababu hakuna mfumo ambao unakuwa kama mtaala wa Wakristo katika Kumwamini Kristo.

Ukweli ni Kwamba Kumwamini Kristo kunaambatana na mambo yafuatayo:-

1. Kujua Asili ya Kristo Kabla ya Mwili  ( Uzao wa Ibrahimu). Hapa ndipo imani thabiti sawasawa na ahadi hufanyika)

2. Kujua uhalisi wa Maisha ya Kristo Duniani ( Neno kufanyika mwili, yaani ufunuo wa uhalisi wa umilele wa Kristo kwa mwanadamu)

3. Kujua Mfumo mzima wa Mauti na Ufufuo wa Yesu ( Hii huthibitisha Ubatizo katika Yesu Kristo na kuonesha jinsi mwanadamu anazaliwa mara ya pili katika Mungu).

4. Urithi wa Utukufu wa Mungu (Hapa mwanadamu hufundishwa kutambua namna ya mfumo mzima wa Ulimwengu ujao utakavokuwa na jinsi ya Kuumiliki)

Katika kila Eneo Fundisho la siku za mwisho limekamilishwa na humsaidia mwanadamu kuona sahihi kwa habari ya Kujiepusha na mfumo mzima Mpinga Kristo kwa ajili ya kuwashinda watakatifu.

Biblia katika kitabu cha Ufunuo inasema “Mnyama alipewa kushindana na watakatifu na kuwashinda”

Katika zama hizi Tuna kidonda ambacho hakijatibiwa na mgonjwa hajayajua maumivu na ukubwa wa kidonda ambacho anacho, huu ni udanganyifu wa kwanza kwa kanisa, yaani kutojua la kujifunza na kulijua kama Njia ya Wokovu itufundishavyo.

#Toba

Fundisho la Siku za mwisho 2

Kitabu cha mwisho katika Biblia ni Kitabu cha Ufunuo.
Kitabu Hiki kimejikita katika kuonesha kinagaubaga  mfumo, majira na nyakati za kanisa, kabla ya kurudi kwa Kristo Mara ya Pili, kabla ya Yesu Kristo kufunuliwa katika mwili, baada ya Yesu Kristo kurudi mara ya pili duniani, lakni mfumo mpya wa Ulimwengu wa ujao katika ufufuo ndani ya Mungu aliye hai.

Mambo haya yote hupambanua Kumjua Yesu ambapo ndio msingi mkuu wa kuelewa Fundisho la siki za mwisho. Yaani Kwa sababu Yesu ndiye chanzo na mfumo unaofanya Nyakati na Majira vifanye kati na viwepo kwa jinsi ambapo vipo hivo kumjua yeye ni kujua Fundisho la kufunuliwa kwake katika nyakati za mwisho.

Ndio maana kitabu cha Ufunuo kinaanza hivi kwa kuonesha mfumo mzima wa ujumbe ambao Upo ndani yake  “Ufunuo wa Yesu Kristo”. 

Maana yake Ni ufunuo wa Yesu Kristo, Shida moja ni kwamba kama kanisa tunafahamu mfululizo wa matukio ya Siku za mwisho mpaka Ulimwengu mpya utakapofunuliwa Bila kuwa na ufunuo wa Yesu Kristo hivo kuchukuliwa na uharibifu kama watu tusio na tumaini.

Unajua Kila jambo limeungamanishwa ( Synchronized) na Mfumo mzima wa Yesu Kristo, Yaani kila hutafsiri ukamilifu wake kwa sababu katika yeye Kila jambo hujishikiza.

Kujua Matukio ya Siku za mwisho hakumfanyi mwanadamu kujiepusha na udanganyifu wa siku za mwisho bali Utambuzi ambao umetokana na Mfumo wa uumbaji yaanj Yesu Kristo ndio humfanya mtu husika Ajikamilishe katika mfumo wa Ufunuo wa nyakati za mwisho.

Kwa Mfano: 

Armageddon ni Vita ya Mema na Mabaya, na ni vita ambayo Mungu mwenyewe ataipiga.

Lakini tafsiri ya mema na mabaya kwa mfumo wa Ufunuo wa Yesu Kristo umekaa katika Asili, ndio maana ya Anguko la Adamu Edeni. Mfumo wake mzima wa asili ulibadilishwa Baada ya kuingizwa kwenye vita hii kinyume cha Taratibu, na moja kwa moja humuingiza mwanadamu katika hali ya uungu ndio maana imesemwa ya kwamba Mungu mwenyewe ataishinda.

Ndivyo ilivyo hata sasa kwa kanisa, kwa sababu ya kutokujua na kusubiri tukio wamepotezwa katika Ufunuo wa Bwana Wao wamtumainio. Yaani kama Vile adamu alivyopotezwa kwa kujuzwa Mema na mabaya kanisa pia limethibitishwa ya kuwa limeangamia katika haya kwa sababu ya Ujinga wa kutokujua Ufunuo wa Yesu Mwenyewe.

Na huku ndiko kushindwa kwa Watakatifu sawasawa na utabiri wa Mtume Yohana.

Amebarikiwa Yeye aliyejitenga kwa Kumtafuta Mungu katika Haki na Usafi wa Moyo.

#Toba

Fundisho la siku za mwisho 3

Kumbuka kuwa kila jambo ambalo limeandikwa katika Biblia au katika Neno la Mungu ni unabii, yaani umefunika ufunuo wa Mungu.

Hivo Si sawa sana kuita Vitabu vilivyoandikwa na manabii kwamba ndiyo vitabu vya kinabii bali maandiko yote ni unabii. Yaani kwanzia kitabu cha Mwanzo Mpaka Kitabu cha Ufunuo, ila.kwa sababu ya kutokuwa na Elimu , basi tumeshindwa kudadavua mfumo husika wa jinsi Biblia inatambua unabii na tafsiri zake.

Kama tukisoma kitabu cja mwanzo mpaka ufunuo basi tutaona jinsi katika kila mstari na kila sura Mungu ameficha Fundisho la kumfikia yeye, ilil mwanadamu atayeshika sana kutazama kweli ya Mungu afikiwe na nuru ya utambuzi na ufunuo.

Namaanisha kuwa Fundisho la siku za mwisho limeanzia kitabu cha mwanzo kabisa, maana hayo yalikuwapo tangia mwanzo ili mwanadamu azione ahadi tokea hapo lakini katika kuzipokea ndio ilibidi wale waliotangulia wasikamilishwe pasipo sisi ambao tulifuata katika Imani.

Kwa Mfano:

Katika Kitabu cha Mwanzo 3, Mungu anamzuia mwanadamu asinyoshe mkono wake ili kula kutoka katika mti wa uzima, asije akala akaishi milele.

Huu ulikuwa ni unabii wa siku za mwisho ambao Hata sasa unatimilika kwa wanadamu wote wanaoishi duniani wakiwa katika mwili.

Mti wa Uzima ni Kristo lakini katika Ufunuo Upitao mfumo mwili,.ndio maana Biblia inasema katika kitabu cha ufunuo ya kwamba ” Heri mtu yule afuaje mavazi yake ili apate kuwa na Amri ya kuuendea mti wa uzima”

Kwahiyo tunaona kumbe kuuendea mti wa uzima ni zao la mtu kuyafua mavazi yake. Lakini Pia Biblia inatuonesha kuwa Adamu angali alikuwa amekwisha kuanguka dhambini lakini alikuwa na Amri ya kuuendea mti wa uzima lakini Mungu akamzuia kwa Vitisho vya Makerubi na Upanga,.maana yake kama makerubi wasingekaa na kuzuia katika Njia ya kuuendea mti wa uzima basi Adamu angeufikia Mti wa  uzima na kula matunda kutoka katika Mti.

Unabii huu ni muhimu kutambulikana katika nyakati hizi maana kwa asilimia kubwa sana ndio mfumo utambuzi wa kizazi katika mambo mengi.

Lengo la Mungu kumzuia Adamu kwanza ni ili Adamu asiutambue uzuri wa Nuru kutoka katika Mti wa uzima wakati akiwa amehaeibiwa Fikra katika Ujuzi wa mema na mabaya, Lakinu ilipasa asubiri kwanza Sadaka ya Agano ya mwanakondoo halafu ndipo apewe amri ya kuuendea mti wa uzima, maana bila hivyo basi kusingalikuwapo ziada ya Sadaka kwa ajili ya upotevu huo.

Utimilifu wa unabii huu katika nyakati hizi unakuja katika Matumizi ya ufunuo wa Yesu Kristo na Hekima yake.

Vikundi vingi vya kiroho duniani tofauti na waamini wa msalaba wa Yesu, wanamkubali Kristo kam mtu mkuu, kama mtu mwenye Hekima, kama Mwana Filosofia Mkubwa , mama Kiumbe wa roho aliyedhihirika katika mwili n.k . Hii inawafanya wafuate mfumo wake wa kimafundisho ambao kwa hakika huwasaidia kuufahanu Ulimwengu wa roho. Lakinil watu hawa hawakubali Kuwa Kristo ndiye mwana kondoo achukuaye Dhambi za Ulimwengu.

Maana yake ni hii, watu hawa hufanya jambo ambalo Mungu alilizuia Katika Kitabu cha mwanzo kwa mtu wa kwanza Adamu. 

Kwa hakika wataishi milele lakini katika mfumo giza uliyofanywa na Nuru ( Kama vile lucifer alivyo hata sasa) yaani alikuwapo katika nuru na hata sasa ana maarifa ya Nuru lakini si uzao wa Nuru.

Basi unaposikia haya na Ujitwike Msalaba wako umfuate Kristo Yesu.

#Toba

Fundisho La siku za mwisho 4

Tukifahamu Kupambanua maandiko basi ni mwanzo mwema wa kuokoka na Ubadhilifu ambao unapatikana kwa wote wenye mwili katika nyakati hizi za Utimilifu wa yote ambayo yanatakiwa kuwapo ili moyo wa mwanadamu uhakikishwe katika Yesu Kristo.

Kuna namna Mbili za kupambanua utilimilifu wa Neno Mungu katika yeyote yule ambaye amelifunua katika kweli.

Yaani kama Biblia inavyotamka, “Mungu alimpa Musa kujua Njia zake na wana wa Israeli Matendo yake”

Lakini pia Yesu Kristo anatuonesha kuja kwa Makristo na Manabii wa Uongo.

Zaidi sana Katika Kitabu cha Waebrania tunaoneshwa Njia ya kuzirithi ahadi ya kwamba ni katika Imani na Uvumilivu.

Njia ambazo maandiko hutafsiriwa ili basi yazae Nuru ndani ya mwanadamu , ni katika Njia mbili Njia ya Utambuzi wa Andiko katika Tukio na Njia ya Utambuzi wa andiko kama Mfumo wa ukuaji wa roho ya mwanadamu.

Kwa Mfano:
Pasaka ni Tukio ambalo huonesha kuhamishwa kwa mwanadamu kutoka katika utumwa na kuhamishwa kuingia katika utawala wa Mungu. 

Pasaka huitwa pasaka baada ya kuthibotoka kuwa vigezo vya kufanya pasaka vimefikiwa.

Ndio maana Yesu Kristo anaitwa Pasaka wetu kwa sababu ya kutokuwa na hatia kwawe, hivyo yeye huwafanya wanadamu wote kuikumbuka Pasaka katika Tukio kutokana na Mfumo wake wa ndani wa kutokuwa na hatia ambao ndio Pasaka halisi.

Maana yake ni hii mwanadamu anaposema ya kuwa anasherekwa Pasaka , maana yake kuna mambo mawili ambayo yanatakiwa kukumbukwa ndani yake, Ni kweli atasheherekea Pasaka katika Utimilifu wa tukio katika mwili lakini pia ni lazima Akumbuke kuwa anatakiwa asherekehe pasaka kwa yeye kuhamishwa kafika mfumo ambao ndio hufanya pasaka yaani kwa kukidhi vigezo vya Utimilifu kama ilivyokuwa kwa Bwana Yesu Kristo.

Haiwezekani kwa pasaka ya mfumo wa ndani kufanyima kama ukamilifu haukufanyika, yaani kama ambavyo haiwezekani kumtoa mwanakondoo asiye mkamilifu kwa ajili ya Pasaka ndivyo ambavyo haiwezekani Kwa mwanadamu kuila pasaka halisi pasipo kuwa kamili kama Vile Yesu.

Ndio maana Biblia inasema baada ya Yesu Kristo kukamilishwa yeye alifanyika Mjumbe wa Agano la Milele.

Lakini zaidi Paulo anatuonesha kwene Waraka Kwa wafilipi ya kwamba ” Anatamani kufananishwa na kufa kwa Yesu kristo” 

Ni muhimu kwa kanuni kuzingatiwa katika Mfumo wa ukamilifu wa roho na nafsi ya mwanadamu ili Kweli ya Mungu ithibitike.

Kumbuka kila Kazi itapimwa kwa Moto, Heri ile  ambayo katika ukamilifu wa siri ya Mungu ilithibitishwa katika Ukamilifu ndani ya Yesu Kristo na kukubaliwa.

#Toba

Recent Posts

Leave a Comment

Contact Us

We're not around right now. But you can send us an email and we'll get back to you, asap.

Not readable? Change text. captcha txt