Neno la Mungu katika Siri (The word of God in a Paradox)

Mithali 25:2

NI utukufu wa Mungu kuficha jambo; Bali ni utukufu wa mfalme kuchunguza jambo

Neno na Mungu limeandikwa kwa Siri kubwa ili Mungu awasadie wanadamu katika Mambo yafuatayo.

1. Kuwasaidia wasiingie Ulimwengu wa roho bila kuhakikishwa

2. Kuwasaidia waingie katika Ulimwengu wa roho kwa utambuzi binafsi katika Mungu kwene Ufunuo wa Neno

Kanisa linatakiwa kukaa na Kujifunza kwa namna hii tu bila kuchanganya na Tabia mwili katika kuwa na uhitaji juu ya yale ambayo neno linaweza likafanya.

Hili ni jambo la Msingi sana maana ndilo hufanya kazi ya Msalaba kwa mwanadamu. 

Pamoja na Haya , Wanadamu tumekuwa Sio wajuzi wa neno katika Ufunuo kwa Sababu ya kukosa Elimu ya ufunuo na hivo kufisha utendaji kazi Wa Fikra ya mwamini katika Kumfikia Mungu kwa kuijua Siri ya Mungu ndani yao wenyewe.

Umakini na jitihada  katika Kufumbua Siri ya Mungu ambayo ni njia ya kutufikisha katika Nuru yake ya milele imefishwa na Uzito wa Kongwa la Uhai ambao hatukujua kwanini tunao, hivo hatukuthamini nafasi ya kuwapo katika Nyumba hii ya udongo, tumefikiri kuwa Uhai ni nafasi ya Kutumia uweza wa Mungu ambao hatukujua Chanzo chake  katika Hekima, Ufahamu na Maarifa. #Katika hili Pia #Mungu #atatuhoji.

Hata kwa Mapigo ya kuzidi Mwanadamu amekataa Kumfuata Mungu maana Hafahamu namna ya Kumfuata yeye, lakini nafasi na muda wa toba haujapunguka maana Walio na Nia ya  Kufunuliwa kwa Yesu Kristo wanafaidi haya katika kweli yote na katika usafi wa Fahamu zao, Hawajapoteza thamani.

#Toba

Recent Posts

Leave a Comment

Contact Us

We're not around right now. But you can send us an email and we'll get back to you, asap.

Not readable? Change text. captcha txt