Wito wa wanafunzi wa Kristo ni kubadilishwa hata kuingia patakatifu pa patakatifu na kukaa hapo ili kufundishwa na Mungu mapenzi yake ili basi Mungu apate kujulikana katika mioyo yao sawasawa na kusudi la uumbaji tangia awali.

Lakini pia Msalaba wa Yesu Kristo , unampatanisha Mungu na mwanadamu , kwa agano la kuileta roho ya mwanadamu katika patakatifu pa patakatifu. Ni vema sana kujua picha halisi ya Agano la msalaba, ili wale walioupokea msalaba wapate ufahamu wa kipimo cha ukuaji na uhakika wa badilisho la asili kufikia Kimo cha ukamilifu wa Kristo Yesu.

Mungu amtuelezea kwa usahihi sana na kwa uangalifu mambo haya ili macho yetu yasitiwe giza katika zama hizi za Ufunuo wa jambo lile ambalo liliandaliwa kwa miaka zaidi ya 1000 ili tunapofunuliwa katika hilo tusipotee bali tuwe na uzima hakika.

Jambo la Msingi sana kulitazama.
Biblia inasema katika kitrabu cha Ufunuo ya kwamba ‘ NAO WAKAMSHINDA KWA DAMU YA MWANA KONDOO NA NENO LA USHUHUDA WAO , AMBAO HAWAKUPENDA MAISHA YAO HATA KUFA.”

Kwa hapa natamani niongelee vitu viwili tu ambavyo humfanya mwanadamu afikie halisi ya patakatifu pa patakatifu au afikie ujuzi wa siri ya Mungu na hekima katika eneo hili ambayo ufunuo wa yeye Mungu wa milele hufanyika,
Damu ya Mwana kondoo.

Lazima tuone katika jicho la kiutambuzi kuhusiana na Biblia kutumia Mwana kondoo katika kutafsiri wokovu wa mwanadamu.

Kwa sababu kama tukiangalia kwa umakini tutafahamu haya ,  kila sadak ailikuwa na utambulisho wake katika kufanya uapatanisho kati ya Mungu na mwanadamu. Yaani sadaka za ngombe, mbuzi, kondoo , ndege na mwana kondoo.

Hivo jambo la kwanza ni kutambua aina ya sadaka ili kuweza kutambua aina ya Wokovu na kipimo chake katika Mungu.
Lakini jambo ambalo nataka kuliongelea hapa ni kuhusiana na Damu ya mwanakondoo ambayo humpa mwanadamu uhalali wa kuingia patakatifu lakini si kuingia patakatifu papatakatifu.
Nimesema kuwa inampa uhalali wa kuingia patakatifu papatakatifu lakini si kupaingia patakatifu papatakatifu. Ndiyo maana ni Damu ya mwana kondoo na Neno la ushuhuda.

Neno la ushuhuda si mambo ambayo Mungu ametutendea katika maisha yetu bali ni mfumo mzima wa kiutambuzi wa kumjua mwana wa Mungu. Ushuhuda huu ndio huachilia mfumo mzima wa Damu ya Mwanakondoo kuthibitisha kibali ambacho kipo ndani yake katika kumruhusu mwanadamu kupaingia patakatifu pa patakatifu. 

Yaani , Nafsi ya Mwili ipo ndani ya Damu, hivo ushuhuda wa Kristo moja kwa moja hufafanua uhalisi wa nafsi ya Kristo ambayo ndiyo damu yake, , hivo kuachilia nafasi ya mtu husika kuingia katika makutano ya Mungu na mwanadamu. Lakini ikumbukwe kuwa damu ya  mwana kondoo huwa haitumiki katika kunyunyiza patakatifu pa patakatifu bali ya Mbuzi kwa ajili ya Israeli na Ngombe kwa ajili ua kuhani. 
Kama unajua kanuni ya Mungu katika kumrudisha mwanadamu katika hema yake basi ni muhimu sana kuwa na Neno la ushuhuda yaani ujuzi wa kweli katika fumbo za Mungu ili basi Agano la Msalaba Lithibitishwe na Ufunuo wa Yes Kristo ndani yako.

Mungu akubariki sana.

Recent Posts

Leave a Comment

Contact Us

We're not around right now. But you can send us an email and we'll get back to you, asap.

Not readable? Change text. captcha txt